Imesasishwa: 03 Oktoba 2026 · Kagua gharama na confirmation ya sasa kabla ya kutuma.
Chagua shughuli na lengo la card
Anza kwa kuchagua Harusi, Send-off au Shughuli nyingine, kisha Mwaliko au Shukrani. Wording na design zitafuata uchaguzi huo. Mwaliko una RSVP na entry pass yenye expiry ya lazima; Shukrani ina ujumbe, signature na picha bila RSVP, QR au scanner. Kutoka main invitation, tengeneza card ya shukrani iliyounganishwa na uchague wazi guests wote valid, walioverifyiwa au contacts zako. Kila lengo la card lina delivery history yake. Invitation Card Preview ya WhatsApp inapatikana sasa kwa mialiko ya Harusi/Send-off; aina/lengo nyingine mpya zinatumia SMS hadi WhatsApp templates ziwekwe. Cards na entry passes zilizopo hazibadilishwi.
Account na policies
Thibitisha signup kwa chaguo la OTP ya email/SMS linalopatikana. Hakikisha email na simu kwenye profile ni sahihi. Version ya policy ya lazima ikihitaji kukubaliwa, isome na ukubali kabla ya kuendelea. Client huingia kwa email/password; admin ana ukaguzi wa ziada wa OTP kwa device.
Deposit na salio
Fungua Deposit, weka kiasi na uende kwenye malipo salama ya ClickPesa. Fuata maelekezo ya malipo hapo. Salio huongezwa baada ya malipo kuthibitishwa, si kwa kufungua checkout tu. Kagua reference, status, invoices na balance transactions kabla ya kuanza malipo mengine. Available balance hutumika kwa campaigns mpya; reserved balance hushikiliwa kwa utumaji ulioidhinishwa. Bei na ada zilizo kwenye review ndizo zinazotumika.
Kuandika na kuthibitisha SMS
Chagua Sender ID iliyoidhinishwa. Ongeza recipients kwa manual, saved list au Excel/CSV. Chagua sheet na heading row, map simu/jina na custom fields zinazohitajika, kisha kagua rejected na duplicate records. Gusa tags zilizopo kuingiza placeholders kwenye message. Counter ya characters/encoding/segments ni makadirio; preview ya kila recipient huhesabu message yake binafsi. Hifadhi na kagua draft, gharama na recipients, kisha tumia confirmation ya mwisho kutuma au kuschedule. Kutengeneza draft hakutumi ujumbe.
Kutengeneza invitation card
Chagua SMS, WhatsApp au zote mbili. SMS inahitaji Sender ID iliyoidhinishwa na message editable yenye private link ya card; WhatsApp hutumia template iliyoidhinishwa ya Invitation Card Preview inayopatikana na inahitaji opt-in ya recipients. Weka design, details za shughuli, picha, location/directions, RSVP na muda wa mwisho wa matumizi ya card ambao ni lazima. Ruhusu guest allocation ikihitajika na ujaze idadi inayoruhusiwa kwa kila recipient. Single/Double ikiruhusiwa, 1 itaonekana SINGLE na 2 DOUBLE; Single/Double kwenye import hubadilishwa kuwa 1/2. Kagua card, WhatsApp na opened-link previews, hifadhi draft, kisha review na confirm kutuma.
Picha na preview ya card
Limit ni 12 MB kwa kila picha. Composer hujaribu kupunguza/compress picha zinazokubalika kabla ya upload, pamoja na zilizovuka limit. Optimization au upload ikikataa, soma error, hifadhi draft na ubadilishe au upunguze picha hiyo kabla ya retry; si kila file linaweza kupunguzwa kwa mafanikio. Moments huenda kushoto kwenye loop kila sekunde tatu. Preview ya ndani ya mwenye card haihesabiwi kama mteja amefungua card. Card ya mgeni huonyesha jina, code na idadi iliyoruhusiwa, si status ya matumizi chini ya QR.
Repeat, retry na delivery reports
Tumia Send again kwa guests/cards/links zilezile, Send to selected guests kwa baadhi ya watu, au Add guests kuongeza wapya ndani ya invitation hiyo. Add guests ina Excel/CSV upload na mapping. Duplicate invitation hutengeneza draft ya shughuli tofauti yenye history mpya. Utumaji wa kwanza na batches za nyongeza hudhibitiwa kwenye main invitation; main campaigns zina unique IDs na batches zina sub references. Retry failed inaruhusu SMS, WhatsApp au zote mbili na review ya SMS editable. Channels zilizofaulu au pending hazirudiwi, hivyo eligible count inaweza kuwa sifuri. Draft/queued/sent/delivered/read/card opened ni tofauti: sent ni provider amekubali, si uthibitisho kwamba imefika.
Kuscan card na kuingiza wageni
Fungua Scan card kwenye dashboard, ruhusu camera na uscan QR. Mfumo hutambua invitation ndani ya access ulizonazo kama owner au ulizopewa. QR isipatikane, tumia entry code ya characters nne kwa herufi kubwa/namba. Access ya staff inaweza kutambuliwa kupitia simu/email ya account iliyounganishwa. Scan inasoma mgeni; kagua details, weka wangapi wamefika na ubonyeze Verify. Idadi haiwezi kuzidi nafasi zilizobaki. Watu wa group wanaweza kufika pamoja au tofauti. Scanner huwa green ikiwa haijatumika, yellow ikiwa partial na red nafasi zote zikitumika. Card iliyo-expire au revoked haiwezi kuthibitishwa. Linda private scanner/staff links na uondoe access isipotakiwa tena.
Contribution registers na records
Tengeneza register yenye jina kwa harusi, send-off au shughuli nyingine, pamoja na tarehe na details. Account moja inaweza kuwa na registers nyingi. Mwenye account pekee ndiye anasimamia records hizi binafsi. Jaza au import majina, simu, ahadi na paid; edit kadri malipo yanavyobadilika. Mfumo huhesabu remaining na kuruhusu search, filter, sort na export. Hii ni register ya kumbukumbu, si huduma ya kupokea michango. Kiasi huonekana kwa comma bila decimal.
Contribution messages, templates na ratiba
Chagua Sender ID iliyoidhinishwa na utumie SMS default au template yenye jina. Unaweza kuedit template, kuupdate iliyopo au kuhifadhi mpya; pia unaweza kuhifadhi message unayoandika kama template kabla ya kuendelea. Tumia tags zilizopo kama {name}, {register_name}, {event}, {pledged}, {paid}, {remaining}, {deadline} na {payment_instructions}. Chagua audience kama wenye remaining balance au selected records, kisha review na send now au schedule. Weekly reminders hutumia kiasi na eligibility vilivyopo wakati wa kutuma. Salio lisipotosha, run inahitaji hatua na account alert hutengenezwa; kuongeza salio pekee hakutumi contribution reminder automatically. Kagua Sending History na uthibitishe ujumbe tena.
Cards za walioqualify kwenye michango
Set thresholds za paid amount kwa Single na Double. Tengeneza au unganisha invitation design moja kutoka kwenye register, ihifadhi, rudi Contributions na uchague walioqualify kabla ya review ya kutuma. Card setup pekee haitumi cards. Cards hizi hutumia main invitation iliyounganishwa na guest/QR records zake badala ya invitation tofauti kwa kila batch. Contribution records zinaeditwa manual; kagua eligibility na gharama kabla ya confirmation.
Kutumia Mobile App
Home, Campaigns, Invitations na Contributions hufungua features za shared workspace. Gusa logo kurudi Home; floating button ya chini hurudisha nyuma. More ina tools nyingine na help. Ruhusu camera kwa scanner na tumia file upload kwa imports zenye mapping. Screen isipoload, kagua connection na reconnect; kagua draft/report iliyopo kabla ya kusubmit tena. Connection error pekee haithibitishi kama message imetumwa au haijatumwa. Details ambazo hazijahifadhiwa si sawa na server-saved drafts.
Admin na Policy Management
Admin tools hutegemea permissions za account. Super Admin Policy Management ina acceptance status ya clients, versions pending, history ya kila client, muda uliorekodiwa (EAT), IP na browser/device user agent. Export history ya client kwa CSV yenye PA record references. Kagua versions za zamani/mpya kwa Kiswahili na Kiingereza na makadirio ya client impact kabla ya confirm publish. Published content haiwezi kueditwa na acceptance records za mwanzo hubaki. IP si uthibitisho wa eneo halisi na user agent si uthibitisho wa hardware. Taarifa za zamani zisizorekodiwa huonyeshwa hivyo.