Omba kufuta account au data
EnglishNyanza Flash SMS, inayoendeshwa na Nyanza Flash Limited, inakuruhusu kuomba kufuta account na data zake, au data maalumu bila kufunga account.
Namna ya kutuma ombi
Jaza fomu hapa chini ukitumia email ya account yako. Huhitaji kurudisha app kwenye simu au kuingia. Msimamizi wa faragha atawasiliana nawe kuhakiki umiliki kabla ya kufuta chochote. Ukiwa umeingia, unaweza kutuma ombi lililohakikiwa kwa kuweka password yako tena kwenye Account settings.
Tunalenga kukamilisha maombi yaliyohakikiwa ndani ya siku 30. Tukihitaji muda zaidi kwa sababu ya mgogoro, wajibu wa kisheria au muamala unaoendelea, tutakueleza sababu na muda unaotarajiwa. Usitutumie password au OTP.
Data zitakazofutwa
Kufuta account kunajumuisha profile na taarifa za kuingia, sessions na vifaa vinavyoaminika, contact lists na imports, maudhui ya ujumbe na recipients, kadi na majibu ya wageni, picha/music ulizopakia, na records za michango za account yako, isipokuwa records chache zilizoelezwa hapa chini. Links za kadi na staff access zitazimwa. Tutaomba pia service providers wafute data panapohusika. Ujumbe uliokwisha kufika hauwezi kuondolewa kwenye kifaa cha mpokeaji.
Kwa ombi la data maalumu, taja contacts, campaigns, kadi, uploads au records za michango zinazofutwa. Account yako itabaki wazi. Tutakueleza records chache tunazopaswa kuhifadhi.
Huhitaji kununua huduma au kufunga account mwenyewe kuomba kufutwa. Staff watasaidia kushughulikia wallet balance, malipo yanayosubiri au campaign ambayo haijatumwa kabla ya kukamilisha ombi. Kusimamisha account au kutoka si kufuta account.
Records chache zinazobaki baada ya kufuta account
Sera ya kampuni: records muhimu za malipo, miamala na invoices, ushahidi wa security/kukubali sera, na record ndogo ya ombi la kufuta data, huhifadhiwa hadi miaka 2 baada ya kufuta account au kufunga ombi. Staff wenye ruhusa pekee wanaweza kuziona; hazitumiki kwa matangazo. Agizo maalumu la kisheria linaweza kuhitaji muda zaidi; tutakueleza records zinazohusika, sababu na muda badala ya kuhifadhi data zote bila kikomo.
Maombi ambayo umiliki haujahakikiwa huisha baada ya siku 90; tuma upya ikihitajika. Backups za kawaida za server huisha ndani ya siku 14. Data iliyofutwa hairudishwi kwa matumizi ya kawaida; backup ikirejeshwa, maamuzi yaliyohakikiwa ya kufuta data lazima yatekelezwe tena. Service providers wanaweza kuwa na wajibu wao wa kisheria wa kuhifadhi records, ambao tutaueleza unapohusika.
Ushahidi uliopakiwa wa manual payment kwa kawaida huondolewa siku 30 baada ya kuidhinishwa/kukataliwa; hii ni tofauti na records za miamala.